Makamu wa rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanznaia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza
mkandalasi wa ujenzi wa mtaro wa kupitishia maji machafu wakati
alipotembelea eneo la Buguruni kwa Mnyamani leo Machi 23, 2015 kwa ajili
ya kukagua maeneo yaliyoathirika kutokana na mafuriko ya mvua
zinazoendele kunyesha jijini Dar es Salaam.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo juu ya
hatua zilizokwishachukuliwa na Serikali, kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi, wakati Makamu alipotembelea eneo la Buguruni Kwa
Mnyamani lililoathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea
kunyesha jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo hilo
baada ya kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo kwa wakati wa
Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam, leo machi 23,
EmoticonEmoticon