Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwahutubia washiriki
wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na
Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere jana Jijini Dar es Salaam na kuhusisha washiriki kutoka nchi 19
wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya lugha ya kiswahili.
Rais wa Kilimanjaro Dialogue
Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na washiriki wa Tamasha la Kimataifa
la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi kutoka
kwa Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz wakati wa
Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kushoto
akifurahia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakionyeshwa na vijana wakati
wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni jana jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili
kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt.
Fenella Mukangara.
Washiriki kutoka nchi 19
wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea katika Tamasha la
Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue
Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar
es Salaam.
Wanafunzi kutoka shule za Feza
wakiburudisha wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni
lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika
Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam na kuhusisha
washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya
lugha ya kiswahili.
…………………………….
Na Lorietha Laurence na May-Zuhura Simba -Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameeleza kuwa lugha ina
mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa itakuzwa sambamba na
maendelao ya teknolojia.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha
la Kimataifa la Lugha na Utamaduni na kufafanua kuwa tamasha hilo
limeonyesha kukua kwa lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi
yetu tangu kupatikana kwa uhuru.
“Mkusanyiko wa leo umeanzisha safari ndefu ya kukuza lugha yetu
ya Taifa toka ngazi za chini hadi za kimataifa, hivyo Tanzania
imefarijika kuwa mwenyeji wa shughuli hii muhimu “alisema Mhe. Dkt.
Mukangara.
Aliongeza kuwa kwa upande wa serikali ya Tanzania imechukua
hatua mbalimbali ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya
kufundishia kuanzi shule ya Msingi hadi Elimu ya Juu.
Dkt. Mukangara ametoa wito kwa vijana kujifunza Kiswahili na
kuitumia lugha hiyo kuweza kujipatia ajira kwa kutangaza utumiaji wa
bidhaa za lugha na utamaduni ambazo zina thamani kubwa kiuchumi.
“Lugha ni sawa na kiwanda ikitumiwa vizuri italeta ajira kwa
jamii husika na kutumika kama lugha ya kufundisha wageni mbalimbali
wanaokuja nchini na hata nchi za nje kwa kuipa hadhi ya kuzungumzwa
sehemu mbalimbali” alisema Mhe. Dkt. Mukangara
Kwa Upande wa muandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Rais wa Asasi
za Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Ali Akkiz amesema kuwa kupitia
tamasha hilo wameweza kutangaza vivutio mbalimbali vya kiutamaduni vya
jijini Dar es salaam na Zanzibar.
“Kwa kweli watoto wamefurahi kushiriki katika tamasha hili kwa
kuweza kutembelea sehemu zenye vivutio vya utamaduni pamoja na historia
najua wataondoka na taswira nzuri ya kutokuisahau nchi ya Tanzania”
alisema Bw. Akkiz
Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni ni la kumi 13
kufanyika ambalo limeshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi
18 kutoka katika nchi 19 na nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili
kwa mara ya kwanza.
EmoticonEmoticon