Makamu wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akishuka
kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma
Makamu wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiambatana
na wenyeji wake baada ya kuwasili mjini Musoma.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa baada ya kuwasili mjini Musoma.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza wimbo wa Tanzania uliokuwa unaimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisangula.
Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala,
akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (katikati), ramani ya Mradi wa
Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini
Musoma. Kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal kuzungumza na wananchi kwenye eneo la mradi.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal,
akizungumza na wananchi.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu
Aseri Msangi na kushoto ni Waziri wa Maji, Prof. Maghembe.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal
(katikati) akikata utepe wa Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto kwake ni Balozi wa
Ufaransa nchini, Melika Berak na viongozi wengine wa chama.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal
akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Uboreshaji wa Hudumu ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma.Kushoto ni Waziri wa Maji,
Prof. Jumanne Maghembe na katikati ni Balozi wa Ufaransa nchini Melika
Berak.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa
Maji, Nadhifa Kemikimba akimuonesha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal
teknolojia ya kusafisha maji kwa kutumia mifupa.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Maji Kitaifa
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal akimpa
kikombe Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji
wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo ikiwa ni moja ya zawadi
zilizotolewa kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Maji.
……………………………………………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO, Musoma
MAKAMU wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohgamed Ghalib Bilal amesema kuwa
kila ahadi ya Serikali iliyotolewa itatimizwa ili kuhakikisha kuwa
inaacha kazi nyepesi kwa viongozi watakaokuja katika kuendeleza
maendeleo ya Tanzania.
Dkt. Bilal aliyasema hayo kwenye
kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani ambayo kitaifa
yamefanyika mkoani Mara yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Mandeleo
Endelevu.
Katika kilele cha Maadhimisho
hayo, Dkt. Bilal aliweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa
Uboreshaji wa Hudumu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Musoma
ambao utagharimu Shilingi Bilioni 44 hadi kukamilika kwake.
“Tumewaahidi kupata maji na hilo
tutatekeleza.Kila ahadi ya Serikali itatimizwa swali ni muda na wakati
lakini kwa kweli hatukusudii kuwaacha njiani, mambo tuliyosema
tutayafanya ili tuwaachie watakaokuja kazi nyepesi ya kuendeleza
maendeleo ya nchi yetu” alisema Dkt. Bilal.
Mradi huo mkubwa wa maji
unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2015 ambapo Dkt. Bilal alisema
mradi huo utakapokamilika itaipatia Manispaa ya Musoma maji ya uhakika
kwa asilimia 100.
Aliongeza kuwa mafanikio ya mradi huo pia ni kuongezeka kwa
uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 10,000 za sasa kwa siku, hadi
mita za ujazo 36,000 kwa siku.
Dkt. Bilal alitoa rai kwa wananchi
wa Manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara kutunza mradi huo na miradi yote
inayoendelea kutekelezwa ili iendelee kuwasaidia wananchi na vizazi
vijavyo.
“Na juu ya haya yote, ni msisitizo
katika utunzaji endelevu wa mazingira yetu ili yaendelee kutuhifadhi.
Aidha, teknolojia za uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa ni
maeneo ambayo yatatuhakikishia kwamba tunakuwa na huduma endelevu ya
rasilimali ya maji” alisema.
Alisema Tanzania haina budi kuwa
na mikakati ya makusudi kukabiliana na changamoto hizo, jambo ambalo
Serikali imeanza kulifanyia kazi.
Alifafanua kuwa uhaba wa maji na kutopatikana kwake kwa uhakika kunaleta athari mbaya katika shughuli zote za kiuchumi.
“Majanga yanayohusiana na maji
kama vile, mafuriko na ukame kwa kiwango kikubwa ni maafa yanayojitokeza
mara nyingi katika sehemu mbalimbali duniani hivi sasa” alisema Dkt.
Bilal na kupngeza kuwa:
“Vifo, uharibifu wa mali, makazi
na miundombinu vina athari kubwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja,
kikundi, jamii na hata Taifa”
Hivyo, alitoa wito kwa wadau wote
kuunganisha nguvu pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za
mabadiliko ya hali ya hewa kwani, mabadiliko hayo yana athari kuanzia
kwenye kupungua kwa misitu na vyanzo vya maji.
Alitaja athari nyingine kuwa ni
kupungua kwa rasilimali za maji juu na chini ya ardhi; kuathirika kwa
ubora wa maji ya kunywa; hadi kukua kwa utoaji wa gesi ya ukaa.
Hata hivyo alisema, Serikali ya Tanzania itaendeleza juhudi
za kuhakikisha inawafikishia wananchi maji safi na salama katika maeneo
ya nchi ambayo yamekosa huduma hiyo.
Aliwakumbusha wananchi kuwa wana
jukumu kubwa la kutunza vyanzo vya maji popote pale vinapopatikana na
kwamba wana kubwa kwenu wananchi ni kutoa mchango unaostahili katika
usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji.
Akimkaribisha Dkt. Bilal, Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema wizara yake itajitahidi na
kufanya kila linalowezekana ili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu
maji yatoke mjini Musoma na wananchi wafurahie huduma hiyo.
Alisema katika kipindi cha
Maadhimisho ya Wiki ya Maji, viongozi mbalimbali walishiriki katika
kukagua miradi ya maji na kutembelea wilaya zote za Mara na kuweka mawe
ya msingi na kuzindua miradi ya maji ambayo imekamilika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji ya Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Musoma, (MUWASA) Mhandisi Said Gantala alisema mradi
huo unajengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya
Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Alisema mradi huo unajumuisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji,
chujio, mtambo wa kisasa wa kutibu maji na ujenzi wa matenki mapya
mawili yenye mita za ujazo 5,500.
Aliongeza pia kuwa, ujenzi huo utajumuisha ujenzi wa mfumo mpya wa mabomba ya usambazaji maji na ujezni wa miundombinu mingine.
“Mheshimiwa mgeni Rasmi Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika
lake la AFD kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Ulaya
(EAD) wamekubali kufadhili mradi wa kuondoa majitaka katika manispaa ya
Musoma” alisema Mhandisi Gantala.
Naye Balozi wa Ufaransa nchini Melika Berak alisema kuwa
amefurahishwa na ushirikiano anaoupata kutoka Serikali ya Tanzania
katika kuhakikisha wanapunguza tatizo la maji nchini.
Katika kilele cha maadhimisho hayo ya 27 ya Wiki ya Maji
Duniani, washiriki wa maonesho katika maadhimisho hayo walipewa vyeti
vya kushiriki na zawadi za vikombe kutokana na makundi washiriki.
EmoticonEmoticon