MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wameanzisha mipango kabambe ya kukabiliana na wadai sugu kwa kuanza kuwafungia wateja wote mita za luku ambazo zitawalazimu kulipia kabla ya kutumia.
Ambapo
mamlaka hiyo inadai kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa Taasisi za
kiserikali na baadhi kwa makampuni binafasi kitendo ambacho kinapelekea wao
kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea ya kukusanya fedha.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka hiyo, Salum Shamte wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji
ambapo kimkoa yalifanyika kwenye kata ya Pongwe yaliyoambatana na uzinduzi wa
Jengo la watoa huduma la Mamlaka hiyo.
Alisema kuwa
hali hiyo itaweza kuisaidia mamlaka hiyo kukusanya fedha za madeni kwa wakati
kitendo ambacho kitawawezesha kuweka mipango imara itakayowapa maendeleo
ikiwemo kuongeza ufanisi mzuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Njia hii ya ufungaji wa mita za luku za
Maji kwa wateja wetu itatusaidia kupata ufanishi katika ukusanyaji wa mapato
yetu hivyo tumeziagiza mita za majaribio ambazo zitaanza kufungwa kwa wale
wadaiwa sugu “Alisema Shamte.
Aidha
aliwataka watumishi wa mamlaka hiyo wenye tabia ya kushirikiana na wateja kuiba
maji kuacha mara moja kwani watakaob ainika hawatavumiliwa watahakikisha
wanachukulia hatua kali ili kuweza kukomesha vitendo hivyo.
“Mtumishi ambaye utabainika kushirikiana na
mteja kuiibia mamlaka kwa kuwaunganishia maji kinyemele nakuambia
hatutawavumilia lazima tutawachukua hatua kali kwani tusipofanya hivyo
tutaendelea kupata hasara “Alisema Shamte.
Kwa upande wake,Mkuu
wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho alisema
kuwa wataendelea kuisaidia mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga(Tanga Uwasa)ili kuhakikisha inapata fedha zote wanazoodai kwenye Taasisi
Sugu ili ziweze kuwasaidia kuendeleza mipango yao.
“Tutahakikisha ninashirikiana nanyi
kuhakikisha wadaiwa sugu wa madeni kwa kuisaidia mamlaka lengo likiwa kuweza
kuzipata fedha hizo kwa ajili ya mipango yenu “Alisema RC Magalula.
Hata hivyo
alitoa wito kwa wateja wanaodaiwa madeni na mamlaka hiyo kulipa mapema kabla
hawajachukuliwa hatua kali.
Mwisho.
EmoticonEmoticon