Waziri
wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango
wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto)
mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Daktari
Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika
uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Waziri
wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Mjumbe
wa Bodi ya ZOP Yahya Mohammed Slim akitoa maelezo kuhusu Jumuiya hiyo
inavyotoa huduma za kijamii vijijini katika usinduzi wa kuwapima usikivu
watoto wachanga.
Wafanyakazi
wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga
wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
baadhi
ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto
wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.