Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu
na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea
mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake
cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na
Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith
Medson.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama
toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu
toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto
Damiano (wa pili kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili
kushoto) na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga
kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa
ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama
baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus
Gaudio wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto
Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri
Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi
ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es
salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo ya matumizi ya
kitabu cha uanachama toka kwa Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw
Joseph Sanga kulia, wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha
uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Kati ni Makamu Mwenyekiti
wa ushirika huo Bw. Deodatus Gudio.PICHA NA IKULU
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na uwepo wa vyama vya
Ushirika vya Akiba na mikopo (SACCOS) katika taasisi na idara za
serikali, akisema kuwa hilo ni jambo la maana kwa kuwa inatoa fursa kwa
watumishi kuwa na kipato cha ziada kitachosaidia kuwaletea ahueni
kwani mishahara pekee haikidhi matakwa yao yote.
Amesema
SACCOS ni
kama
benki ya mtu mnyonge, na kusisitiza kwamba mifuko ya aina hiyo
inaposimamiwa vizuri faida yake kwa wanachama ni kubwa sana kwani humpa
mtumishi ahueni na kumfanya afanye kazi kwa moyo na bila wasiwasi ama
usongo wa mawazo.
Balozi
Sefue ameyasema hayo Jumanne Machi 3, 2015 jioni alipokuwa akiongea na
uongozi wa Ikulu SACCOS,
uli
omtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es salaam kumkabidhi rasmi kitabu
chake cha uanachama kufuatia kujiunga kwake na ushirika huo.
“Mishahara
yetu ndani ya utumishi wa umma haitoshi kukidhi mahitaji yetu yote, kwa
hiyo mipango yote hii ya SACCOS, Mfuko wa Rambirambi na Mfuko wa
Ushirika
iliyopo hapa Ikulu
inafanya maisha ya mtumishi yawe na ahueni sana na kumfanya afanye kazi
kwa moyo.
“Hayo
ni mambo ambayo nayaamini sana na nayaunga mkono; na naamini hata Mhe
Rais mwenyewe anayaunga mkono na ndio maana amekuwa mwepesi kujiunga na
ushirika ”, amesema Balozi Sefue baada ya kukabidhiwa kitabu namba 2 na
Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio. Kitabu namba
moja amekabidhiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Awali,
mshauri Mkuu na Mlezi wa Ushirika huo wa Ikulu, Bw. Joseph Sanga,
alimfahamisha Katibu Mkuu Kiongozi kwamba mifuko ya SACCOS, Ushirika wa
Nyumba na Rambirambi ya watumishi wa Ikulu iko imara na inaendelea
kunufaisha wanachama wake kwa ufanisi.
Bw.
Sanga amesema malengo makuu ya mifuko hiyo ni kuleta ustawi kwa
watumishi na kwamba wote wanaelewa kuwa mikopo ya SACCOS yao sio kwa
ajili ya kununulia chakula ama mavazi bali ni ya kuwekeza kwenye miradi
itayowaongezea kipato.
“TUnataka
kwenda mbali zaidi kwa kushirikiana na mfuko wetu ya Ushirika wa Nyumba
ambo tayari umepeleka maombi ya ardhi kwa wanachama wake ambapo viwanja
vikipatikana tuna mategemeo ya kuwapa mikopo kuvununua. Mpango huu una
faida kwani ni wa amana kubwa na riba ndogo”, alisema Bw. Sanga
alipokuwa anafafanua kuhusu mipango ya Ikulu SACCOS.