Baada
ya klabu ya Manchester United kupwaya katika nafasi ya kiungo siku za
hivi karibuni, klabu hiyo chini ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal yenye
maskani yake katika dimba la Old Trafford, ipo mbioni kumfukuzia kiungo
wa klabu ya Borrusia Dortmund Ilkay Gundogan.
Gundogan
ambaye amekuwa akifanya vizuri katika mechi za karibuni akiwa na klabu
yake ya Dortmund sasa ameonekana Lulu kwa Manchester United huku klabu
hiyo ikifanya jitihada za kumpeleka Old Trafford.


EmoticonEmoticon