Sehemu
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali
katika mitaa ya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima
Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni
Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya
Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mbezi
Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga na wa kwanza
kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin kutoka Makao Makuu ya
Magereza, Dar es salaam.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya
kutembea katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi
wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza Bagamoyo Mkoa wa Pwani,
Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi wa Magereza Jamhuri
Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
Maafisa
na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa
katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015. Wa sita kutoka mbele
ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomiah Hamis na wa mwisho ni
Mkaguzi wa Magereza Abas Mikidadi.
Maafisa
na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa
katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya
viungo baada ya kutembea na kukimbia katika viunga vya Manispaa ya
Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6,
2015.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipata kifungua kinywa
baada ya mazoezi mazito ya maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro
ifikapo Machi 6,2015. Maafisa hao wako kambini eneo la Gereza Karanga
mjini Moshi.
Baadhi
wa washiriki wa Kilimanjaro Marathon Machi 1, 2015 mbio ambazo baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walishiriki ikiwa ni
maandalizi ya kupanda Mlima Kilimanjaro mnao Machi 6, 2015. Picha zote
na Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja