MAMLAKA ya Mamlaka ya
Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema kuwa
haitasita kuwafutia leseni pamoja na kuvifungia vyombo vya majini
vitakavyoendelea kutoa huduma hiyo bila kufuata sheria ikiwemo kukaguliwa na
kupewa cheti cha ubora.
Kauli
hiyo ilitolewa na Ofisa Mfawizi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Walukani Luhamba
wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema kuwa vyombo vingi
vinavyotoa huduma kwenye maeneo hayo vimekuwa hazikaguliwi hali ambayo ni
hatari kwa usalama wa watumiaji.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuwa na vyombo vilivyokaguliwa na kufanya kazi zao
kwa kufuata sheria zilizopo hapa nchini jambo ambalo litapunguza ajali za mara
kwa mara zinazotokana na ubovu wa vyombo hivyo.
Luhamba
alisema kuwa watahakikisha kila chombo ambacho kinatoa huduma zao kwenye eneo
la majini wanakuwa na leseni za kutoa huduma kwenye maeneo hayo pamoja na
vyombo hivyo kufanyiwa uhakiki wa kina.
“Tunasema kuwa wamiliki watakaoshindwa kupeleka vyombo vyao kukaguliwa
hatutawaacha tutahakikisha kuna kula nao sahani moja ikiwemo kuvifungia vyombo
hivyo kwani hatutakubali wafanya kazi bila kukaguliwa “Alisema Luhamba.
Aidha alisema kuwa lazima ufike
wakati wamiliki kuacha kufanya kazi kwa mazoezi kwa sababu hali hiyo inaweza
kuwapa matatizo wananchi wanaovitumia hasa nyakati inapojitokeza ajali.
Hata hiyo alisema mamlaka hiyo kwa
kushirikiana na idara nyengine watashirikiana kwa pamoja ili kuweza kupambana
na wale wote ambao watashindwa kufuata sheria hizo kwa kuwachukulia hatua.
EmoticonEmoticon