WANANCHI MICHEWENI WATAKIWA KUTOKUWA NA TAMAA YA FEDHA NA KUUZA ASHAMBA YAO MARA MBILI

February 27, 2015

jabu 
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana akila kiapo kuchukuwa majukumu ya kuwa mkuu wa wilaya ya Micheweni.
PICHA NA MAKTABA
……………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana ameitaka jamii kuepukana na tamaa ya fedha kwa kuuza mashamba yao watu zaidi ya mmoja ili kuepusha kutokea kwa migogoro ya ardhi katika maneo yao .
 
Amesema kuwa migogoro mingi ya ardhhi inayojitokeza siku hadi siku inasababishwa na jamii kwua na tama ya fedha hali ambayo inawafanya kukosa uwaminifu na hivyo kujikuta wakisababisha kuwepo na migogoro .
 
Akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika shehia ya Makangale Jimbo la Konde , Mkuu huyo wa Wilaya ameshusha presha za wananchi hao baada ya kuahidi kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo .
 
Amekiri kuwa shehia ya Makangale na Tondooni zinakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi na kuwataka wananchi wa shehia hizo kumpa ushirkiano ili aweze kutekeleza azma yake ya utatuzi wa migogoro kwa lengo la kulinda amani na utulivu uliopo hapa nchini .
 
“Migogoro ya ardhi inaweza kuepukika iwapo kila mmoja atajiepusha na vitendo vya tamaa ya fedha na kuuza maeneo kwa zaidi ya mtu mmoja , lakini cha msingi naomba mnipe ushirikiano ili niweze kufanikisha leng la kuimaliza migogoro hii ” alifahamisha .
 
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka kamati ya maadili pamoja na polisi Jamii katika shehia ya Makangale kufuata taratibu za kisheria katika kukusanya mapato yatokanyo na ada ya magari yanayoingia kwenye ufukwe wa Vumawimbi kwa kuhakikisha wanatoa risiti .
 
Amesema kuwa ni vyema  Kamati ya Maadili pamoja Polisi Jamii kushirikiana na taasisi za serikali zinazohusika na masuala ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo Halmashauri ya Wilaya na kupanga mikakati ya mapato katika ufukwe huo .
 
“Tayari tumepokea taarifa kutoka kwa wananchi kwamba hawapewi risiti wanapo fedha katika ufukwe huo na kwamba hali inaweza kuitia dosari Serikali hiyo ni vyema wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushirikiana na taasisi husika ” aliongeza .
 
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya hiyo Ahmed Khalid Abdalla amefahamisha  kwamba ili kuepusha migogoro ya ardhi Serikali ya Wilaya itaendelea na utaratibu wa kukutana na wananchi pamoja na wawekezaji ili kutafuta suluhu kwa faida ya umma .
Katibu Tawala amewataka wawekezaji kuacha kupora ardhi za wananchi , na badala wawashauri  na kuwepo makubaliano ya pande zote zinazohusika .
“Pamoja na jamii kuwa na tama ya fedha lakini kwa upande mwengine wawekezaji nao wamekuwa wakisababisha migogoro kwa kuchukua maeneo ya wananchi bila ya ridhaa za wenyewe” alifahamisha .
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwepo na migogoro ya ardhi zaidi ya tano (5)  katika shehia ya Makangale na Tondooni ikiwemo inayohusu wawekezaji  na jamii , Viongozi wa Serikali  na wananchi pamoja na wananchi wenyewe kwa wenyewe.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »