Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Makatibu Kata wa CCM, Wilaya
ya Nachingwea mkoani Lindi leo. Katika mazungumzo hayo yaliyojumuisha
Makatibu Kata zaidi ya 30, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao
kuhakikisha wanazunguka katika kata zao kuhakikisha wanawahamasisha
wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya maandalizi ya
kuipigia kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Katikati
Meza Kuu ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mussa Liliyo akifuatiwa na
Mwenyekiti wa Makatibu Kata hao, Ally Napepa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
mkoani Lindi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu
wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Mussa Liliyo wakati alipokuwa
akimwakikishia mbunge wao, kuwa timu ya Makatibu Kata wake wamejipanga
kikamilivu katika kuwahamasisha wananchi jimboni humo kujitokeza kwa
wingi kujiandikisha kwa ajili ya kuipiga kura Katiba iliyopendekezwa
pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
mkoani Lindi, Mathias Chikawe (wanne kushoto-mstari wa mbele) akiwa
katika picha ya pamoja na Makatibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
jimboni humo baada ya kuwapa somo makatibu hao la kuhakikisha
wanawahamasisha wananchi kujitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya
kuipiga kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Picha zote
na Felix Mwagara.
EmoticonEmoticon