EFM YAANDAA HAFLA YA VALENTINE

February 12, 2015

Team Nzima ambayo inaongoza kipindi cha ya sports headquaters ambacho kinaruka kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa saa tatu mpaka saa sita mchana(Kweli wamechizika). EF2 
 Kala Pina akiweka pozi la nguvu na mchizi wake Swebe.Unaweza kumsikiliza Swebe katika kipindi cha Gurudumu ambacho kinarushwa kila siku Jumatatu mpaka Ijumaa Saa Sita mchana mpaka saa Tisa,akiwa na mwanadada Safia,Manganje pamoja na RDJ X5. EF5 
Meneja Uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole akiwa na mchizi wake Samira Kiango.Samira ni mhariri msaidizi katika chumba cha habari cha EFM Redio na pia ni mtangazaji wa habari.
Francis Mhando ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Sports Headquaters akiwang’ara na machizi wake kutoka Canada.
………………………………………………..
Kila mwaka,tarehe 14 Februari,watu duniani kote huadhimisha siku ya wapendanao duniani. Kama ilivyo ada,wengi wetu tumezoea kuadhimisha siku hiyo na aidha mume,mke au mpenzi. Ila kituo cha redio cha 93.7 EFM, kinawapa nafasi ya kipekee wasikilizaji wao kuchagua mtu ambaye wao ndio wanamuona kama mchizi wao. Meneja Uhusiano wa 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole,amesema mchizi wako sio lazima awe mpenzi wako,bali anaweza kuwa kaka,dada,jirani,bosi wako au hata mama mkwe wako,wote hao wanaweza kuwa mchizi wako. “Sio lazima kila mwaka tufanye mambo yale yale,tumeona tufanye mabadiliko kidogo,alisemea meneja huyo. Siku ya “wewe ndio mchizi wangu”,itafanyika pale Msasani Beach Club,siku ya tarehe 14 mwezi huu wa February mwaka 2015,ambapo itahusisha wasanii kama vile Mesen Selecta (Mzee wa kanya boya),Recho Kizunguzungu,Msaga sumu,Snura, Sir Juma Nature,RDJ Majay akiwa na Zungu the drama na wengine kibao. Kanky alisema kwamba ukija na mchizi wako,kutakuwa na zawadi kubwa sana kutoka kwa DJ Majay na Zungu the drama. “Tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi,kwani watangazaji wote watakuja kupiga picha na kuongea na mchizi wa EFM 93.7.Bado tunaendelea kuwaleta wasikilizaji wetu karibu na sisi,kama mnakumbuka mwaka jana,tuliwaletea tamasha la “Mziki Mnene”,ambapo tulipata nasafi kubwa ya kujumuika na washabiki wetu kwa mda wa miezi mitatu mfululizo,na tukawaahidi kuwaletea mambo mengi mbele ya macho yao”,alisema meneja uhusiano huyo. Kanky alisema kuwa,zawadi nyingi zitatolewa kwa mtu na mchizi wake na pia kutakua na michezo mbali mbali ambayo itafanyika siku hiyo ya 14 February 2015. Aliendelea na kusema kwamba hii sio tamasha bali watu waje na machizi wao kuja kuchizika,ni kuanzia saa kumi jioni mpaka watakapo choka.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »