NA BASHIR NKOROMO.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari
Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo,
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM
katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na
presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu
mwaka huu.
Amesema,
ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo
vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na
Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi
gani.
"Chama
hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za
wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika
chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha
kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya
taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", alisema Nape.
Alisema,
kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa
CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo
akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu...
huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona
kama anatosha", alisema Nape.
"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", alisema.
HABARI KATIKA PICHA
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiingia katika ofisi za Kampuni
ya Habari Corporation Ltd, kendelea na ziara katika vyombo vya habari
aliyoianza wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma
wa CCM, Godfrey Chongolo
Nape akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Habari Corporation Denis Msaky baada ya kuingia chumba cha habari
Nape
akisalimiana na Matinyi ambaye ni mmoja wa wahariri katika kampuni hiyo
ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai na
Dimba
Napa kisalimiana na Mhariri wa Msanifu wa Habari wa Mtanzania Hamis Mkotya.
Nape akiwa katika chumba cha habari cha Mtanzania
Nape akitazama picha iliyomvutia katika chumba cha habari cha Mtanzania, ambayo alionyeshwa na Msaky.
Picha
yenyewe ni ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa,
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Muasisi wa Habari Corporation,
Jenerali Ulimwengu
Nape akionyeshwa chumba cha habari cha chenye mkusanyiko wa madawati mbalimbali ya magazeti ya Mtanzania Rai na Dimba
Nape akisalimiana na Mhariri wa habari za Siasa Sarah Mosi
Nape akisalimiana na Mhariri wa habari wa Mtanzania, Bakari Kimwanga
Nape akisalimiana na John Mlinda
Nape akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Usanifu
Nape akiwa katika picxha ya pamoja na wasanifu wa kurasa
Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda akimkaribisha Nape
Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda, akitambulisha kwa Nape uongozi wa magazeti ya kampuni hiyo.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati
akizungumza na uongozi wa New Habari Corporation Ltd, hasa kuhusu
masuala ya wagombea Urais
Nape akizungumza zaidi
Nape akizungumza mambo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Corporation, Hussein Bashe baada ya mazungumzo ya ndani
Wakuu wa New Habari Corporation wakiagana na Nape nje ya ofisi za kampuni hiyo
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa na Mhariri Mkuu wa
Mwananchi, Bakari Machumu baada ya kuwasili kwenye ofisi za Kampuni ya
Mwananchi Communications Ltd leo
Bakari Machumu akimkaribisha Nape ofisini kwake. Kushoto ni Chongolo
Nape na Machumu akiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi na The Chitizen
Nape akizindikizwa na Machumu wakati wakienda ukumbini kwa ajili ya mazungumzo zaidi
Nap0e akizungumza na uongozi wa magazti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd
Nape akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd
Nape akimpatia zawadi ya kalenda ya CCM, Bakari Machumu, mwishoni mwa mazungumzo
Haya kwaherini mbaki salama...
"Mimi pia nipo hapa" Angetile Oseah akimwambia Nape baada ya kukutana wakati akiondoka ofisi za Mwananchi Communication Ltd.
Nape akiagana na Bakari Machumu mwishoni mwa mazungumzo. Picha na Bashir Nkoromo
EmoticonEmoticon