Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi
Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya
mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng’ong’o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma
Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo
na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge
wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George
Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge
kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia
amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima
ili ziweze uwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.
Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu
mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya
kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia alisema kuwa serikali
inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika
kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.
“Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine
muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na
ni muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa
katika eneo la kazi”alisema Nkamia
Aidha alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari
ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao
ya kazi na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia
wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika.
Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila
shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna
aliye juu ya sheria .
Hata hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa
maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo vitambulisho na
mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni
mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.
Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa
ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa
mbugeni wakati wowote kuanza sasa.