Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Hassan
Khatib Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Wete Hassan Khatib Hassan amesema kuwa
hatakuwa tayari kufanya kazi na asasi za kiraia ambazo zitakuwa
zinafanya kazi kwa mlengwa wa chama cha siasa kwani hazitakuwa na
mwelekeo mzuri .
Akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la
Mtabwe waliofika Ofisini kwake kujitabulisha , amesema kuwa siasa ni
sumu ya mafanikio ya Jumuiya na kwamba Jumuiya nyingi zimekuwa
zikishindwa kufikia malengo yake kutokana na Viongozi kuzihusisha na
masuala ya kisiasa .
Aidha Mkuu wa Wilaya ameelezea kusikitishwa na kitendo cha
uharibifu wa mazingira katika Jimbo hilo hasa vitendo vya ukataji wa
miti na kuitaka Jumuiya hiyo kuhakikisha kuwa maeneo ya wazi ambayo
yameathirika kwa kukatwa miti ovyo yanarejeshwa katika hadhi yake kwa
kupandwa miti
Amefahamishwa kuwa asasi ya kiraia zina nafasi kubwa katika
kufanikisha udhibiti wa uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko
ya Tabianchi iwapo zitakuwa tayari kutoa elimu kwa jamii
inayowazunguka.
Amesema kuwa katika kufanikisha suala la uhifadhi na
udhibiti wa uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji ovyo wa miti
asasi za kiraia zinatakiwa kuwa mstari wambele kuwaelimisha wananchi
athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayotokea siku hadi siku.
.
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza haja kwa Jumuiya hiyo kukaa
pampja na asasi nyingine ambazo zinafanya kazi sawa na Jumuiya hiyo ili
kuondoa suala la migongano katika utendaji wa kazi zao .
“Tunatambua kwamba asasi za kiraia zinanafasi kubwa katika
kudhibiti suala la yharibifu wa mazingira na mafanikio zaidi
yatapatikana iwapo mtakuwa tayari kushirikiana na Jumuiya nyingine
ambazo zina malengo sawa na ya Jumuiya yenu ” alifahamisha .
Naye Diwani wa Wadi ya Mtambwe Hamad Mjaka Bakar amesema
kuwa lengo Jumiya hiyo ni kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira pamoja na
kutafuta njia muafaka za kutatua kero zianazo wakabili wananchi wa
Jimbo hilo .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo
hilo Said Massoud amesema kuwa uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokea
katika Jimbo hilo ni ukataji ovyo wa miti pamoja na uvuvi wa chaza wa
kutumia vijembe .
Amesema kuwa uvuvi wa aina hii umekuwa ukichangia sana
matendo ya uharibifu wa mazingira na kuongeza kwamba Jumuiya tayari
inaendelea na kampeni zake za utoaji wa elimu kwa wananchi ili kudhibiti
vitendo hivyo .
“Vitendo hivi ni lazima tukiri kwamba vipo katika Jimbo letu
la Mtambwe na hasa vya ukataji miti ovyo pamoja uvuvi wa chaza kwa
kutumia vijenmb vidogo vidogo na hili tunaendelea kupambana nalo na muda
mfupi wananchi wataepukana nalo ” alieleza.
Hivyo Jumuiya hiyo imeiomba Serikali kuweka msukumo katika
kufanikisha kuyadhibiti matendo hayo kwa kuwahakikisha kwamba
wanaosafirisha miti mibichi wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria .