Kutengeneza
uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo
hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza
kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo
haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu
marafiki zetu.
1. Nakupenda: Ni kitu
rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa
unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha
au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.
2. Nilikuwa nakuwaza: Ni
muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu
moja.Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho
kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?:
Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za
kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi
kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu
zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa
pamoja.
4. Unga mkono maamuzi
mazuri ya mpenzi wako: Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga
mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia
afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile
hisia kuwa una mtu mwingineupande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka.
Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma
yake kutaimarisha uhusiano wenu.
5. Mwambie mpenzi wako kuwa
Umependeza: Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi
kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa
anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya
ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
6. Samahani ni neno zuri
kwa mpenzi wako: Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine
hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa
sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba
msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa
kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio
kosa lako.
7. Hakuna kama wewe: Mpenzi
wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi
hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye ni
bora na hakuna kama yeye.
8. Napenda mawazo yako
Picha: StudioMwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe
kuwa unaona anaakili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.
9. NakuheshimuKama ulivyo
uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi wako. Mpe
nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo yanayokutatiza. Mtu
anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na salama, vitu ambavyo ni
muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10. Napingana na hilo:
Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale
usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila
kitu na hakuna mwanamke anayetakakuzaa watoto na mwanaume asiye na
msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye
mawazo na matendo ya kila mmoja.
Kuwa na maoni
yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wakomtazamo tofauti
kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa
ameliwaza.11. Usiku mwemaTunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni
rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka
bahari, hivyo hakuna kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’
mwema.Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia
inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa
kama mmejibizana,