VODACOM NA TFF ZATILIANA SAINI MKATABA WA KUIDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

August 12, 2015

Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa wakijiandaa kutiliana saini mikataba yao. Kulia anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo, Boniface Wambura.
Malinzi na Twissa wakibadilishana mikataba huku Wambura (katikati) akishuhudia.

Malinzi akisistiza jambo kwenye mkutano huo.
Twissa akijibu maswali ya wanahabari hawapo pichani.Mkutano ukiendelea.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom leo imetiliana saini na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF mkataba wa kuendelea kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kipindi kingine cha miaka mitatu. Kampuni hiyo imeendelea kuidhamini ligi hii baada ya kuidhamini kwa miaka minane mfululizo iliyopita.
Mkataba huo umetiwa saini kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Makao Makuu ya Vodacom yaliyopo Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »