Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu
Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakipiga makofi pamoja na wajumbe wengine muda mfupi
baada ya kuingia katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mjini
Dodoma tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM leo jioni.
(Picha na Freddy Maro)
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM
Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na
Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha wakijadiliana jambo muda
mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM
Dkt.John Pombe Magufuli wakiteta muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha
Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.