Baadhi ya vijana kutoka shule
mbalimbali wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa leo
jijini Dar es Salaam na kuhusisha mashirika mbalimbali ya mataifa
yanayofanya shughuli za vijana yakiwemo UNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS
DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE STOPES, pamoja na PSI.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (wapili kulia) akipokea maandamano ya vijana (hawapo pichani)
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani
iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
na wapili kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi.
Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto
ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
Kijana ambaye ni mwanachama wa
asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) Bw. Hesein Melele
akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano
lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa
ya vijana duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi
leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya
kimataifa ya vijana duniani.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi
akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na vijana wakati wa maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni
Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara hiyo Prof. Hermas Mwansoko
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(kushoto) akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
Baadhi ya vijana wakifuatilia kwa
makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka vikundi mbalimbali
wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka vikundi mbalimbali
wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka vikundi mbalimbali
wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka vikundi mbalimbali
wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Vijana
Bi. Amina Sanga (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa
ya vijana duniani yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw.
James Kajugusi.
Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo