Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akitoa hotuba kwa niaba ya
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha
Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimtukuku Shahada ya Uzamili
katika Uchumi wa Maendeleo Amina Salum Mwanja wakati wa mahafali ya 28
ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini
Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mwanafunzi
wa mwaka wa pili anayesomea Shahada ya kwanza ya Mipango ya Usimamizi
wa Mazingira katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Azizi
Mshau akimweleza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet
Mbene namna bora ya kundaa mipango miji inayokuwa rafiki kwa mazingira.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akiagana na Mkuu wa kwanza wa
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga
mara baada ya sherehe ya mahafali ya 28 ya Chuo hicho.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene () akiwa katika picha ya
pamoja na wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) mara
baada ya mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP)
iliyofanyika jana mjini Dodoma.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- Dodoma)
Na Eleuteri Mangi- Dodoma
Serikali
imesema inaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuweka mazingira
rafiki kwa kuboresha mifumo ya ajira katika sekta ya umma na ile ya
binafsi ili kujenga uchumi wa kisasa unaozalisha ajira pamoja na
kuwawezesha vijana wasomi nchini kujiajiri.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kwa
niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) yaliyofanyika jana mjini
Dodoma.
“Ninafarijika
sana kusikia vijana wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini wameweza
kuonesha njia kwa kuweka kwa vitendo waliyojifunza kwa kuanzisha miradi
ya kiuchumi katika sekta ya kilimo kama njia ya kujiajiri” alisema
Mbene.
Naibu
Waziri huyo aliwahakikishia vijana hao kuwa Serikali ipo tayari kusaidia
juhudi hizo kupitia fursa mbalimbali za kuwasaidia vijana na
wajasiriamali kupitia fursa zinazoendelea kutolewa na Serikali.
Naibu
Waziri Mbene alisema kuwa ili kutekeleza lengo hilo, Serikali inaendelea
kuhamasisha uwekezaji katika kilimo, uchimbaji wa madini na uwezo wa
kuongeza thamani mazao yetu yanayozalishwa.
Mbene
aliongeza kuwa maeneo yote hayo yanatoa fursa nyingi kwa wahitimu vijana
nchini kuajiriwa katika ngazi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na
kujiajiri.
Akimkaribisha
Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa
Chuo Dkt. Razack Lokina alitoa kilio cha chuo hicho cha kuomba kada ya
mipango kupewa nafasi stahili katika mfumo wa ajira Serikalini.
Akifafanua
suala hilo Dkt. Razack alisema kuwa kukosekana kwa kada ya Mipango
kumesababisha kazi za kada hiyo kutotekelezwa ipasavyo kwa kiwango cha
ufanisi unaotakiwa.
Aidha,
Dkt. Razack alisema kuwa taaluma ya Mipango inamtayarisha Afisa Mipango
ambaye jukumu lake ni kubuni, kupanga, kufuatilia, kutathmini, kuratibu
shughuli na rasilimali katika maeneo ya Mipango ili kufikia malengo ya
maendeleo ya jamii kusudiwa tofauti na taaluma ya Uchumi ambayo
inamuandaa Afisa kuwa na jukumu mahususi la kuchambua ili kutoa hali
halisi ya mazingira ya kiuchumi kisekta.
Kwa
upande wake Chuo hicho Constantine Lifuliro alisema kuwa wahitimu wa
chuo chake wameandaliwa vya kutosha wapo tayari kutoa huduma katika
nyanja mbalimbali kwenye maeneo waliyojifunza hasa katika kuandaa,
kusimamia, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo
katika maeneo mbalimbali watakayofanyia kazi.
Naye
mhitimu Baltazar Ngeze, kwa niaba ya wahitimu wa mwaka huu wa chuo hicho
aliushukuru uongozi wa chuo kwa kuwaandaa vema kwenda kutekeleza
majukumu yao ya taaluma ya Mipango katika jamii watakayokuwepo.
Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1,909 waliotunukiwa tuzo zao katika kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.
Kati
ya wahitimu hao, wapo wanaume ambao idadi yao ni 1,003 sawa na asilimia
52 ya wahitimu wote na wanawake idadi yao ikiwa ni 906 sawa na asilimia
48 ya wahitimu wote.
Idadi
hiyo ya wahitimu wa mwaka huu inaonesha wameongezeka wahitimu 63 sawa na
silimia 3.4 zaidi ya wale waliohitimu masomo yao mwaka jana 2012/2013
ambao walikuwa 1,846 kati yao wakiwa wanaume 1,037 sawa na asilimia 56
na wanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44.
EmoticonEmoticon