Mdhamini wa Kombe la Mwidau CUF, Amina Mwidau akiwa na wabunge wenzake, Yussuf Salim (Chambani) na Khatib Said Haji (Konde)
Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timu ya Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake.
Kombe la likiwa mezani huku mchezo wa fainali ukiendelea. Na mpigapicha Wetu
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Pangani
Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa
ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka
ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja wa
Mwera wilayani Pangani.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni
wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga
ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika
dakika za awali toka mpira kuanza.
Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha
ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao
matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko .
Hata hivyo kipindi cha pili
Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza katika
dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo
baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli la pili la timu hiyo
lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa
timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku
yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga bao la nne.
Akikabishi zawadi kwa washindi hao
Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC
walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa,
medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku mshindi wa pili ambae ni
Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba, seti moja
ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na
16 zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza kabla ya kuanza
kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya
soka katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali
hapa nchini.
Katika mchezo huo wa fainali
ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said
Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.
EmoticonEmoticon