Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga imeagizwa
kuanza utekelezaji wa utozaji wa faini ya papo kwa papo ya sh 50,000 kwa wale watakabainika kuchafua mazingira.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Magid Mwanga wakati wa kongamano la kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira lililoandaliwa na Shirika la Wanawake la Utunzaji wa Mazingira nchini (YWCA),kupitia mradi wake wa ‘wajibika’.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na afisa tarafa ya
Lushoto,Asha Hazali,mkuu huyo wa Wilaya alisema pamoja na jitihada zinazochukuliwa ikiwemo kampeni ya usafi wa kila mwisho wa mwezi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi wakati wote,bado wako baadhi ya watu ambao kwa makusudi wanakwamisa jitihada hizo.
"Umefika sasa wa sheria kuanza kufanyakazi kwani kama ni suala la elimu limekuwa likitolewa sana na viongozi wa serikali na wanaharakati mbalimbali hivyo kuna kila sababu kwa adhabu kuanza kutolewa"alisema Mwanga .
Akizungumzia kuhusu mpango huo,afisa wa mradi wa
‘wajibika’nchini.Carloline Biseko,alisema kuwa unawahusisha zaidi vijana, ili waweze kujitambua na kushiriki kikamilifukatika kutunza mazingira.
Kwa mujibu wa Biseko ni kuwa sanjari na masuala ya mazingira vijana pia wana elimishwa juu ya masuala ya ujasirialimali ili waweze ili waweze kutumia fursa zilizopo kuzalisha mali nakuondokana na umaskini.
Kongamano hilo liliwashirikisha wasanii na wanafunzi kutoka shule za sekondai za Magamba na Lushoto,ambao walifanya kazi za kusafisha mazingira ya mji na kupanda miti.

EmoticonEmoticon