KIKOSI CHA KMC AMBACHO KIMEIFUNGA VILLA SQUAD MABAO 2-0,MKWAKWANI LEO |
WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI WAKISALIMIANA LEO |
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU ya Soka ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam(KMC) leo imeifunga timu ya Villa Squad "Watoto wa Magomeni"mabao 2-0 kwenye mechi ya Ligi daraja la kwanza iliyochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mabao ya washindi hao yalipatikana kunako dakika za 38 na 67 kupitia kwa wafungaji wake Camara Jongo aliyatumia uzembe wa mabeki wa Villa Squad na kupachika wavuni bao hilo.
Kwenye mechi hiyo bao la pili la lilifungwa na Mohamed Ndonga kwenye dakika ya 67 ambaye alipiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Villa Squad Fadhili Saidi na kujaa wavuni.
EmoticonEmoticon