KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA,FRESSER KASHAI AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI DOLA ZA KIMAREKANA FEKI ZILIZOKAMATWA NAZO WATUHUMIWA HAO |
WATU watatu wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa noti
bandia mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakiwa na dola
za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za
Kitanzania .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai aliwaambia
waandishi wa habari jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17 mwaka huu
saa saba na nusu eneo la barabara ya kumi na sita Kata ya Ngamiani wilayani
Tanga wakati kwenye harakati za
kuziingiza kwenye mzunguko.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Polisi wakiwa
kwenye gari lenye Chasis namba JLg 100037726 ambazo ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa na
noti hizo bandia ambazo walikuwa wamezificha
Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kuwa ni
Julius Kanza(30),kabila Mchaga na Mkazi wa Ubungo,Kenedy Binagi(35) mkazi wa
Sinza na wa tatu ni Ramadhani Saddy(33)
kabila Muha na mkazi wa Mwenge
Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya watuhumiwa hao
kukamatwa walikiri kuhusika na biashara hiyo ambapo wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelekezi wa awali
kukamilika.
Wakati huo huo,Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linaendesha msako
mkali wa kuwatafuta wahusika wa matukio ya mauaji ya Mkulima mmoja yaliyotokea
Kijiji cha Nyadigwa Kata na Tarafa ya Kimbe wilayani Kilindi.
Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo la mauaji hayo lilitokea Novemba 18
mwaka huu majira ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano katika eneo la
kijiji cha Vyadigwa Kata ya Kimbe wilayani humo.
Akizungumzia tukio hilo,Kamanda
Kashai alisema mkulima wa Vyadigwa alikutwa porini akiwa amejeruhiwa maeneo ya
utosini kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana hali iliyomsababishia
kifo chake.
Alisema kuwa mkulima huyo alifariki dunia saa kumi jioni
wakati akiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Kilindi(KKT) ambapo chanzo cha
mauaji hayo bado kinachunguzwa .
EmoticonEmoticon