MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI

November 18, 2014
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 18.11.2014.
  • MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI NA WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI KYELA.
MWANAMUME MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HENRY AMBAKISYE (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KANDETE ALIKUTWA AMEUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MAJINI KATIKA MTO KANDETE NA WATU WAWILI AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA MTO HUO MNAMO TAREHE 17.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANDETE, KATA YA KAJUNJUMELE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
 AWALI MNAMO TAREHE 15.11.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU WAKATI MAREHEMU ANATOKA NGOMANI AKIWA NA MWANAMKE MMOJA AITWAYE KISA KIMA (48) MKAZI WA KAPWILI ALIVAMIWA  NA KISHA KUSHAMBULIWA NA WATU HAO. AIDHA MWANAMKE HUYO BAADA YA KUONA HALI HIYO ALIKIMBIA NA KUTOWEKA ENEO LA TUKIO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA YA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI UTOSINI.  CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA KUGOMBEA MWANAMKE.  KISA KIMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
 Imesainiwa na:
          [BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »