KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA MTAMA

November 18, 2014

 01 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Bernard Membe Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wakati alipowasili katika Kiwalala Kituo cha Ufugaji cha Masister cha Narunyu ambapo ameshiriki kazi ya kukamua maziwa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali lakini pia  kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Katibu mkuu Kinana katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MTAMA -LINDI)3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kukamua maziwa katika kituo cha uugaji cha Masister cha Narunyu Mtama mkoani Lindi wakati alipotembelea kituo hicho.02Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Masister mara baada ya kuwasili katika kituo hicho katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.1 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mtama wakiwa katika kikao cha ndani wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . 7 
Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Maifa Mh. Bernard Membe akizungumza na wajumbe wa mkutano huo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikilizia wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.   18 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. kushoto na Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda wakicheza ngoma za asili ya kabila la Kimakonde wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika kata ya Chiuta jimbo la Mtama mkoani Lindi19 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 24 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Chiuta leo. 23 
Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika kata ya Chiuta leo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »