Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa
nyuki kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles
Ratia katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11,
2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa
nyuki kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles
Ratia katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11,
2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali
iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki
barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
chaArusha ( AICC) Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael na watatu kulia ni
Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akitazama mazao mbalimbali yanayotokana na nyuki
katika maonyesho yaliyokwenda sambambamba na Kongamano la Ufugaji Nyuki
Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC),
Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu na kushoto kwake ni Mhamasishaji wa ufugaji nyuki na usindikaji
asali wilayani Loliondo, Krystern Erickson.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali
iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki
barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
chaArusha ( AICC) Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael na watatu kulia ni
Jacob Edward. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma kabla ya kufungua kongamno la
ufugaji nyuki Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC) Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua Kongamano la Ufugaji
Nyuki Barani Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC) Novemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu vifaa vya kukamulia asali
kutoka kwa watalaam wa Kichina, Huang Hejie (kushoto) na Zhinyong Wang
(watatu kushoto) katika kongamano la Ufugaji Nyuki Afrika lililofanyika
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 11,
2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema
Serikali itaendelea kuyalinda makabila madogo nchini yakiwemo ya
Wahdazabe na Wasandawe ambayo yanategemea rasilmali misitu kwa maisha
yao na ustawi wao.
“Tutakuwa tunafanya makosa kama
tutawanyang’anya rasilmali misitu makabila madogo hapa nchini kama vile
Wahadzabe, Wandorobo na Wasandawe kwani ndiyo rasilami pekee
inayowawezesha wapate chakula cha kutosha,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Novemba 11, 2014) wakati akifungua Kongamano la Kwanza la
Ufugaji Nyuki Barani Afrika la Mwaka 2014 lililoanza leo kwenye ukumbi
wa AICC, jijini Arusha. Kongamano hilo linashirikisha wajumbe 590 kutoka
ndani na nje ya nchi. Nchi za nje zinazoshiriki kongamano hilo ni 24,
ambapo kati ya nchi hizo nchi 12 ni za bara la Afrika.
Kongamano hilo la siku tatu
limeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuwakutanisha
wafugaji nyuki, wafanyabiashara, wataalamu na wawakilishi wa taasisi za
ndani na nje ya nchi ili kujadili njia za kuboresha ufugaji nyuki na
kukabiliana na changamoto za ufugaji nyuki hapa nchini na barani Afrika
kwa ujumla.
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa
Halmashauri na watu wenye maamuzi wasiwasumbue kwa kuwalazimisha
wabadili maisha yao na kutoka kwenye mfumo wa ikolojia (ecosystem) ambao
wameuzoea. “Tusiwabugudhi, tusiwatoe kwenye mfumo wao wa ikolojia.
Tuwasaidie kuwapa teknolojia mpya ili waweze kufuga kisasa na kupata
faida huku wakiishi kwenye mazingira hayohayo waliyoyazoea mpaka hapo
watakapozoea na kuamua kubadilika kwa kubaini kuwa njia zao za zamani
haziwasaidii sana.”
Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki
barani Afrika, Waziri Mkuu alisema ufugaji nyuki umeegemea zaidi katika
rasilimali misitu na kilimo ambapo Afrika kwa asilimia kubwa shughuli
ya ufugaji nyuki hufanyika katika misitu.
“Bara la Afrika lina ukubwa wa
eneo la kilometa za mraba milioni 30.2 na asilimia 20 ya eneo hilo ni
misitu. Asilimia 40 ni misitu ya Savanna ambayo ni muhimu kwa ajili ya
ufugaji nyuki. Mapori haya pamoja na maeneo ya kilimo yana uwezo mkubwa
wa kuzalisha mazao ya nyuki kwa wingi,” alisema Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu ufugaji nyuki
nchini Tanzania, Waziri Mkuu alisema takwimu za Shirika la Chakula la
Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani
Afrika inayozalisha asali kwa wingi (tani 34,000 kwa mwaka), ya kwanza
ikiwa ni Ethiopia (tani 45,000 kwa mwaka).
“Inakadiriwa kuwa Tanzania ina
uwezo wa kuzalisha tani 140,000 za asali na tani 10,000 za nta kwa
mwaka. Lakini ni asilimia saba tu ya uwezo huo ndio huzalishwa. Hii ni
kwa sababu zao hilo limepuuzwa tangu siku nyingi na halijapewa msukumo
unaostahili.”
Alisema sekta ya ufugaji nyuki
ina mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu kwa kumpatia chakula,
ajira na kipato. “Wananchi hunufaika kutokana na mauzo ya asali, nta na
mazao mengine ya nyuki, utengenezaji wa vifaa vya ufugaji nyuki,
kusambaza malighafi za viwandani na huduma ya uchavushaji,” aliongeza.
“Wafugaji wa nyuki katika nchi zilizoendelea wanatumia teknolojia ya kuvuna sumu ya nyuki (bee venom), gundi ya nyuki (propolis), maziwa ya nyuki (royal jely)
na chavua (pollen) ambavyo hutumiwa kama virutubisho na dawa. Tafiti
zimethibitisha kuwa gundi ya nyuki hutibu maumivu ya meno, malaria na
homa ya mifupa(arthritis) na kuongeza kinga mwilini. Sumu ya
nyuki imekuwa ikitumiwa kuongeza nguvu za uzazi, kutibu uvimbe na homa
ya mifupa,” alisema huku akishangiliwa.
Waziri Mkuu aliitaka sekta
binafsi na taasisi za utafiti barani Afrika zifanye tafiti zaidi
katika eneo hili na kuwekeza katika teknolojia ambayo inaweza kuvuna na
kuchakata mazao hayo ambayo yana soko kubwa katika viwanda vya
kutengeneza madawa, virutubisho na vipodozi.
Mapema, akielezea kuhusu
kongamano hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu
alisema Juni mwaka jana, Wizara hiyo ilisaini makubaliano na Shirikisho
la Ufugaji Nyuki Duniani (Apimondia) ili waweze kuandaa kongamano la
ufugaji nyuki barani Afrika mwaka 2014.
Alisema kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni: “Kufuga nyuki kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira na kukuza uchumi” yaani “African Bees for a Green and Golden Economy” litahusisha
mada 88 ambazo kati yake, 45 zitawasilishwa na watafiti wa kisayansi,
26 zitakuwa za majadiliano (roundtable) na 17 zitawasilishwa katika
semina.
Alisema kongamano hilo ni kwanza
kwa sababu ni mara ya kwanza kwa kongamano kama kuandaliwa barani Afrika
kwa kushirikiana na Apimondia kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu species za nyuki zilizopo Afrika na mazingira ya ufugaji nyuko barani humu.
EmoticonEmoticon