TAIFA STARS YAWASILI JOHANNESBURG
Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa
Stars tayari kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa
maandalizi ya mechi dhidi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili
(Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini
Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha
Mart Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho
Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Wakati huo huo, kikosi cha
maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa
ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo
itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa
Stars kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa
kinakutana mara moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na
kucheza mechi moja ya kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
WAAMUZI 23 KUSHIRIKI SEMINA DAR
Waamuzi 23 wa daraja la kwanza
wakiwemo wenye beji la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
wameteuliwa kushiriki semina itakayofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ambayo
pia itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test)
wanatakiwa kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye hosteli ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Wakufunzi wa semina hiyo wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Riziki Majala na Soud Abdi.
Waamuzi watakaoshiriki semina
hiyo ni Ahmed Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles
Peter Simon (Dodoma), Dalila Jafari Mtwana (Zanzibar), Ferdinand Chacha
Baringenge (Mwanza), Florentina Zabron (Dodoma) na Frank John Komba
(Pwani).
Grace Wamara (Kagera), Hellen
Joseph Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Issa
Bilali Ali (Zanzibar), Issa Haji Vuai (Zanzibar), John Longido Kanyenye
(Mbeya), Jonesia Rukyaa Kabakama (Kagera) na Josephat Deu Bulali
(Tanga).
Kudra Omary (Tanga), Martin
Eliphas Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mfaume Ali Nassoro
(Zanzibar), Mgaza Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel Hudson Mpenzu (Arusha),
Soud Iddi Lila (Dar es Salaam) na Waziri Sheha Waziri (Zanzibar).
EmoticonEmoticon