Injinia Dkt Binilith Mahenge awataka watanzania kutumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mazao

November 11, 2014

0 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge akifungua rasmi Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal,itakayofanyika kwa muda wa  siku mbili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
1 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ndg. Sazi Salula (katikati), akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), pamoja na Mkurugenzi Msaidizi – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt.Richard Muyungi katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Washiriki kutoka Nje na ndani ya Nchi wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani). unnamed 
Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki kutoka Ndani  na Nje ya Nchi waliohudhuria katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nch4Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ,kuhusu umuhimu wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Benki Kuu ya Dunia kwa ushirikianao na Ofisi ya Makamu wa Rais. Anayefuatia wa pili kulia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Philippe Dongier (kulia) pamoja na Bw.Vel Gnanendran Mkuu wa Ofisi ya DFID nchini Tanzania.
………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya  na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu. Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam. Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.
Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania  zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira. Aidha alisema kuwa zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika  kuhakikisha utunzaji wa  mazingira unatekelezwa na pia  kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia moja au nyingine.
Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.
Mwisho Waziri Mahenge aliwashukuru Wadau mbalimbali ambao wamehudhuria kongamano hilo kutoka ndani na nje ya Nchi. Akiwasihi sana kuendelea kutunza mazingira na pia aliwaomba watembelee vyanzo mbalimbali vya Utalii vilivyopo Nchini Tanzania ili kukuza uchumi .
Kongamano hilo ni muendelezo ya Mkutano wa New York kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu na limehudhuriwa na washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »