ALIYEKUWA MKUU WA MKOA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GHALAWA KATIKA MOJA YA VIKAO MKOANI HAPA AMBAYE KWA SASA AMEHAMISHIWA MKOA WA DODOMA |
WANAWAKE Mkoani hapa wametakiwa kuwa
sehemu ya kukua kwa uchumi wa Taifa, na kuunga mkono dira ya Taifa 2025,
MKUKUTA na Malengo ya milenia kwa kufanya biashara na ujasiriamali wenye tija
zitakaz waongezea kipato.
Dira
ya Maendeleo ya Taifa 2025 ilianzwa kutekelezwa mwaka 2000 ili kuongoza
harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia
hadhi ya nchi yenye kipato cha kati na kuondoana na umaskini uliokithiri.
Malengo
ni kuboresha hali za maisha ya watanzania, kuwepo kwa kwa mazingira ya amani,
usalama na umoja, Kujenga utawala bora, kuwepo na jamii inayoelimika vyema na
inayojifunza; na Kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka
nchi nyingine.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Luteni (mstaafu) Chiku Ghalawa alipokuwa akifugua kampeni ya Wanawake na
Uchumi kwenye ukumbi wa Naivera Compex, eneo la Bombo Mkoani hapa.
Amesema kwa muda mrefu uchumi wa nchi
umeongozwa na wakulima na wafanyakazi na kwamba wakati kwa wajasiriamali na
wafanyabiashara ni sasa kuwa wachangiaji wakubwa wa pato la Taifa.
Kampeni hiyo imeandaliwa na asasi isiyo
ya kiserikali ya Angels Moment kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto kwa lengo la kuwaonyesha wanawake kuwa si kila
changamoto inaashiria kurudisha nyuma juhudi zao bali ni firsa ya kusonga
mbele kwa kuanzisha mpya yenye ushindani.
Awali Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi, Mahada Erick amesema
pamoja na juhudi nyingi za kumkomboa mwanamke mjasiriamali bado ameendelea
kukumbana na changamoto zilezile kila siku hali inayosababisha wengine kukwepa
biashara na ujasiriamali kwa kuogopa matokeo ya waliotangulia kushindwa.
Licha ya changamoto hizo Mkuu wa Mkoa wa Tanga amewatia moyo wanawake
walioudhuria hafla hiyo wapatao 300 kuwa halmashauri ya Jiji la Tanga imetenga
asilimia 10 ya pato lake kuwanufaisha pamoja na vijana huku akiwasisitizia
wasiwaache kinababa nyuma kwani baadhi yao mkoani hapa hawajishughulishi jambo
ambalo ni fedheha na kugusia maandiko yanayosema asiye fanya kazi na asile.
EmoticonEmoticon