Manchester
City inajiandaa kuzipiga bao Liverpool, Arsenal na Manchester United
kwa kumpa ofa ya pauni milioni 10 kwa mwaka staa wa Borussia Dortmund
mwenye umri wa miaka 25, Marco Reus ili atue Etihad.
Reus
amekuwa bidhaa adimu inayosakwa na klabu kibao za Ulaya zikiwamo pia
Barcelona na Bayern Munich, lakini kwa mujibu wa gazeti la Bild la
Ujerumani, Man City ndiyo inaonekana kudhamiria kufanya kweli kwa kuweka
mezani ofa hiyo kubwa.
Hivi
karibuni Reus alionyesha nia ya kutaka kubaki Borussia Dortmund, lakini
kutokana na klabu hiyo kutaabika katika Bundesliga kwa sasa, staa huyo
atalazimika kufikiria upya mustakabali wake mwisho wa msimu, hasa kama
kikosi cha Jurgen Klopp kitashindwa kufuzu kwa Champions League.
EmoticonEmoticon