Manchester
United inaonekana kukabiliwa na kibarua kizito cha kupigania kumbakisha
kundini kipa wake namba moja, David de Gea, baada ya Real Madrid
kuelezwa kumfungia kazi kuhakikisha anatua Santiago Bernabeu.
De
Gea amekuwa na mafanikio makubwa licha ya United kuwa na mwendo mbaya,
na umahiri wake umewatia mzuka mabingwa hao wa Ulaya kutaka kumsajili.
Kipa
huyo mwenye miaka 23, mkataba wake wa sasa Old Trafford unakwenda hadi
mwaka 2016 na kwa mujibu wa gazeti la Sun la Uingereza, Real Madrid ina
matumaini ya kumtia mikononi kwa punguzo la bei katika usajili wa
kiangazi kijacho kama mbadala wa muda mrefu wa Iker Casillas.
De
Gea – kipa wa zamani wa Atletico Madrid anaaminika kuwa tayari kuhamia
Bernabeu na mabosi wa Real Madrid wanaelezwa kuwa na matumaini ya
kufanikisha dili lao kama Man United itafeli kucheza Champions League
kwa mwaka wa pili mfululizo.
EmoticonEmoticon