MUWSA YASAMBAZA BOMBA ZA MAJI MRADI MKUBWA WA MAJI MTO KARANGA.

November 05, 2014


Mkurugenzi wa Mamlaka  ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (aliyevaa  suti nyeusi) akiwaongoza wanahabari kutembelea mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemichemi ya Mto Karanga.
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Mhandisi Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu ujenzi wa kituo cha kutibu maji katika chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha wanahabari chanzo cha maji kilichopo Mto Karanga .
Wanahabri wakipita juu ya Bomba zilizoanza kusambazwa kutoka katika chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Bomba za kupitisha maji kutoka katika Chemichemi kando ya Mto Karanga zikiwa tayari zimesambazwa kwa eneo kubwa kwa ajili ya kupitisha maji kuelekea maeneo ya Pasua na kwingineko.
Moja ya kiungio cha bomba za maji za nchi 10 kwenda nchi 8 zilizosambazwa toka chanzo cha Chemi chemi ya Maji kando ya mto karanga
Sehemu ya kutolewa hewa katika maungio ya bomba za maji zinazosambazwa kutoka chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Bomba la maji likiwa limepita kando ya Mto Karanga.
Maeneo mengine mafundi walilazimika kuchimba eneo kubwa ili mradi kwepa vipando katika maeneo ambayo Bomba hilo limepita.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika maeneo ambayo bomba hilo limepita.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha eneo ambalo bomba zinazosambazwa kutoka chanzo cha Mto Karanga zitaunganishwa kwa ajili ya kupeleka maji kwa watumiaji.Eneo hilo liko jirani na kiwanda cha Bia cha Serengeti.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

TATIZO la upungufu wa maji katika Manispaa ya Moshi linaelekea kuwa historia ifikapo mwezi Desemba mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa  mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 382.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia maeneo ya Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.
Mhandisi Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.
Amesema mradi huo utasaidia kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa maji kwa mita za ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji ambapo kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia 99.
Amefafanua kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »