Katibu
wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu
alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na
katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa
mdahalo huo, Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba
isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda
mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa katika vurugu hizo na Mzee Warioba
na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju
wakati wa vurugu zilizotokea katika mdahalo wa kujadili rasimu ya
Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jana, ambapo
Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha
kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia
Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu
kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba
kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda
wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo
Makonda
akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa
aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka salama
pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho Amon Mpanju ambaye pia
alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini.
EmoticonEmoticon