Makamu wa Rais wa Afrika Kusini awasili nchini kwa ziara ya siku moja

November 04, 2014


Makamu wa Rais wa  Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa akiteremka katika ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere Jijini  Dar es Salaam.  Mhe. Ramaphosa yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Mahusiano , Mhe. Stephen Wasira kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (Mb), na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi   wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini.  
Mhe. Ramaphosa akilakiwa na Mhe. Wasira mara baada ya kuwasili.
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika mara baada ya kuwasili. 
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Talha Mohammed 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa Matamela alipofika Ikulu kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Ramaphosa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kwa pamoja na Mhe. Wasira wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Rais na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini 
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo.Picha na Reginald Philip

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »