Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kuingia kwenye
gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na
hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama
Mahakama katika kikao chake hicho.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akifafanua
jambo wakati akiwahoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa shirika hilo, James Andilile wakati kamati hiyo, ilipokaa kama
Mahakama katika kikao chake kilichofanyika jana, Ofisi za Bunge, Dar es
Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na
Polisi kwenda kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada
ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa
muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
EmoticonEmoticon