MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ALHAJ MAJID MWANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZIDUZI WA UGAWAJI WA VIATU HIVYO KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUMBULI BEATRICE MSOMISI |
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUMBULI BEATRICE MSOMISI AKIMVALISHA KIATU MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI SONI |
NA MWANDISHI WETU,LUSHOTO.
MKUU wa wilaya ya Lushoto ,Alhaji Majid Mwanga amesifu jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Januari Makamba kwa hatua aliyochukua kwa kuwapatia viatu wanafunzi wote waliopo kwenye shule za msingi katika Halmashauri ya Bumbuli.
Makamba alitoa viatu 48600 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi tisini na saba zilizopo kwenye maeneo mbalimbali kwenye Halmashauri ya Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga .
Lengo la kugawa viatu hivyo ni kuwasaidia kuwaepusha wanafunzi
wanaosoma kwenye shule hizo kuepukana na magonjwa mbalimbali hatarishi ikiwemo tatizo la minyoo hali ambayo inaweza kuwaathiri wakati wa usomaji wao jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma maendeleo yao.
Mkuu huyo wa wilaya alisema jambo hilo linaonyesha jinsi gani Mbunge huyo alivyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu nzuri itakayowawezesha kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi waliopo kwenye shule mbalimbali kwenye halmashauri hiyo.
Alisema mbunge amafanya jambo nzuri ambalo linawatengenezea afya nzuri wanafunzi hao kitendo ambacho kitaongeza juhudi zao za ufaulu kutokana na kuepuka magonjwa ambayo yanaweza kuwakwamisha katika masomo yao ikiwa wataugua.
Aidha aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kutumia fursa ya kuwa na mbunge huyo ili waweze kujiletea maendeleo na kuwataka viongozi wengine walipo wilayani humo kutumia njia alizopita mbunge huyo ili kuweza kuhakikisha wanafunzi wilaya nzima wanapata viatu.
“Jambo hili alilolifanya Mbunge wetu ni kuharakisha maendeleo kwa wananchi wake kwa kuhakikisha wanapata elimu nzuri kwa kuwa katika afya nzuri hivyo juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wengine “Alisema DC Mwanga.
EmoticonEmoticon