MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza amesifu juhudi zinazofanywa na Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) katika kusaidia sekta ya elimu wilayani humo lengo likiwa kupandisha juu taalumu hiyo kwenye shule mbalimbali kwa kuwawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira mazuri.
Mgaza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akipokea msaada wa mifuko 250 ya saruji iliyokuwa na thamani ya sh.milioni nne kutoka kwa mfuko huo wa Pensheni katika makabidhiano yaliyofanyika shule ya msingi Mwakikonge ya jamii ya kimasai wilayani humo.
Mfuko huo wa Pensheni ulitoa mifuko hivyo kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu kwenye shule tatu za msingi wilayani humo ambazo
zinakabiliwa na changamoto hiyo ambazo ni Mwakikonge mifuko 100,Mwakikoya mifuko 100 na Gonja Segoma mifuko 50.
Alisema juhudu hizo zinaonyesha kuwa namna gani mfuko huo ulivyokuwa na malengo makubwa ya kuhakikisha wanachangia maendeleo ya sekta hiyo hasa katika masuala ya ujenzi wa miundombinu jambo ambalo linasaidia kukuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hizo.
Aidha alisema kuwa wilaya hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kila shule inakuwa na miundombinu ya kutosha ikiwemo madarasa ilikuwawezesha wanafunzi kusoma kwa
Aliongeza kuwa shule hiyo ya Mwakikonge ina uhaba mkubwa wa
miundombinu ambayo ilijengwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuwasaidia jamii ya kimasai ili kuweza kupata elimu na kuwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jihudu hizo.
Awali akizungumza kabla ya kukabidhi mifuko hiyo,Afisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Samweli Haule alisema kuwa waliamua kutoka msaada huo ili kuchangia harakati za elimu wilayani humo kwa kuboresha miundombinu.
Aliongeza kuwa baada ya kutoa msaada huo matumaini yao makubwa ni kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora ambayo inaweza kuwainua kiwango cha ufaulu wao hasa katika mitihani yao ya mwisho.
Naye kwa upande wake,Afisa elimu Msingi wilayani Mkinga,Zakayo Mlenduka alisema msaada huo umewafikia wakati muafaka ambapo walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu na kuhaidi kuutumika kwenye matumizi yasiyokusudiwa.
Utoaji wa mifuko hiyo ya Saruji katika shule hizo unatokana na ombi ambalo liliwasilizwa kwenye mfuko wa PSPF na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantuma Mahiza kuwaomba wasaidia masuala ya ujenzi kwenye shule ya mwakikonge inayosomewa na jamii ya kimasai ili waweze kupata elimu bora.
EmoticonEmoticon