Kupitia
Semina za Fursa zinazoendelea kufanyika katika mikoa mbali mbali hapa
nchini, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imekuwa ikitoa Elimu
ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo
ili waweze kunufaika na mafao ya NSSF hususani matibabu bure kwa
mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kupitia SACCOS.
Fursa
nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja
na Pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, msaada
wa Mazishi, Mafao ya Uzazi, mafao ya Kuumia Kazini.
Semina
hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali, wakulima pamoja na watu
mbalimbali waliojiajiri wenyewe na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu
huduma zinazotolewa na NSSF na wengi hujiuga na NSSF baada ya kuona
faida zake.
"Katika
semina za Fursa NSSF inafanya uandikishaji wa wanachama wapya na pia
inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kufahamu mambo mbali mbali
yanayohusu mfuko huo" alisema Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba.
Mpaka sasa NSSF imeshiriki katika Semina ya Fursa katika mikoa ya Geita, Ruvuma, Mbeya na Morogoro.
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba akitoa mada katika semina ya Fursa kuhusu Elimu
ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko huo
ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF hususani Matibabu
Bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kwa wanachama
kupitia Saccos. Semina hiyo ilifanyika mkoani Mbeya hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (katikati), Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa tatu kutoka kulia) wakiwa meza Kuu pamoja na wageni wengine wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Mbeya.
Baadhi
ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya
Fursa iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini Mbeya.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba akitoa mada katika semina ya
Fursa Mbeya iliyodhaminiwa na NSSF kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi
wakazi wa Mbeya.
Afisa
Matekelezo wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa mada kuhusu faida za kujiunga
na NSSF kwa wakazi wa mjini Songea wakati wa Semina ya Fursa
iliyofanyika mkoani Ruvuma.
Msanii
wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwasihi wakazi wa Songea wajiunge na
NSSF ili waweze kupata Fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mafao mbali
mbali ya NSSF kama Mikopo kupitia Saccos, Matibabu Bure, Pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini.
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa pili kushoto), Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (kushoto) wakifuatilia kwa
makini semina ya Fursa iliyofanyika Songea mkoani Ruvuma.
EmoticonEmoticon