Wachezaji
26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda
ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin
itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha
Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini
Ali (Azam).
Mabeki
ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam
(Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo
ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba
(Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna
Chanongo (Simba).
Washambuliaji
ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR
Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane
Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
BONIFACE
WAMBURA
MKURUGENZI
WA MASHINDANO
SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
EmoticonEmoticon