SERIKALI MKOANI TANGA YACHUKUA TAHADHARI MLIPUKO WA UGONJWA WA EBOLA

September 30, 2014


Afisa Afya kutoka Hospitali ya Bombo Bw. Said Ibrahim akifundisha kwa vitendo jinsi ya uvaaji wa mavazi na vifaa maalumu wakati wa kutoka huduma ya kitabibu kwa mgonjwa wa Ebola . Aliyevaa mavazi maalumu ni Dr Nakiete Mchomvu.
SERIKALI  imetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa mgonjwa yeyote mwenye  dalili ya ugonjwa wa Ebora ili aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi kwa watu wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa hatari wa Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma kwa madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga (Bombo).
Kikao hicho ni moja ya jitihada ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa  wa ugonjwa huo hatari ambao sasa  umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.  Vile vile ametoa wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu zao pamoja katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa dhidi ya jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika Mkoa wa Tanga,Mganga  Mkuu wa Mkoa  wa Tanga Dr Asha Mahita amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili kutoa huduma ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni pamoja na eneo la Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga na kituo kingine kipo Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua tahadhali katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro  mpaka wa Tanzania na Kenye na uwanja wa ndege kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na kutambua msafiri mwenye maambukizi ya  Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za jirani na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya, Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka Chama cha Watoa huduma Binafsi za Afya Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo la msingi iwapo Serikali na Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili kudhibiti na kuzuia ebola kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika nchi ya Tanzania.  Historia inaonyesha mwaka 2012  Mwezi wa Julai ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola  magharibi mwa Uganda eneo linaitwa Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virusi na husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha damu.

DSCO4681Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo akifungua rasmi kikao hicho .Kulia  ni Mganga Mkuu Mkoa waTanga Dr Asha. Mahita na Mtendaji Mkuu kutokaChama cha Watoa Huduma binafsi za Afya Nchini, Dr. Samweli Ogillo.

Afisa Afya Mkoa wa Tanga Bw. Magoma akitoa maelezo juu ya ugonjwa wa Ebola
 
Wajumbe wa Kikao wakisikiliza kwa makini
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akizungumza na wajumbe muda mchache  kabla ya Mgeni rasmi kufungua kikao rasmi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo na kulia na Mtendaji Mkuu Kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za Afya, Dr Samweli Ogillo
Mtendaji Mkuu kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Dr Samweli Ogillo akitoa dhana ya ushirikiano baina ya sekta Binafsi na Sekta ya Umma katika kuboresha huduma za afya. Kushoto ni Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Dr Asha Mahita  na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego.
Picha ya pamoja ya wajumbe na mgeni rasmi,Picha na Stori kwa hisani ya tovuti ya mkoa wa Tanga.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »