WIZARA YA AFYA YASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE HOSPITALI TEULE YA TUMBI KIBAHA

September 19, 2014



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakati alipowasili mjini Kibaha kuendelea na ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Katibu mkuu pia anahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuimarisha chama, Katika msafara huo Kinana anaogozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. Kero kubwa iliyojitokeza katika ziara hiyo ni pale Mkurugenzi wa huduma za Afya katika hospitali ya Tumbi Dr. Peter Dattan aliposema Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliahidi kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo(ICU) Lakini ahadi hiyo haijatekelezwa yapata miaka mitatu sasa, Pamoja na kwamba hospitali ya Tumbi Kibaha inapokea majeruhi wengi na wanahitaji tiba maalum kutokana na majeraha mbalimbali yanayosababishwa na majeruhi wa  na ajali, Hospitali ya teule ya Tumbi inapokea asilimia 80% ya majeruhi wa ajali. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBAHA) 2 
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka akitoa maelezo ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha kwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. 4 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo ambali ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha inajegwa mjini Kibaha 6 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akipanda mti katika jengo la ofisi mpya ya CCM wilaya ya Kibaha inayojengwa. 7 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapongeza watoto wa chipukizi baada ya kuimba ngonjera yao mbele yake. 8 
Baadhi ya vijana wa Kambi ya vijana ya UVCCM ya wilaya ya Kibaha wakiimba nyimbo kumkaribisha Katibu mkuu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea kambi yao iliyopo Boko Timiza mjini Kibaha. 11 
 Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakishiriki katika shughuli za usafishaji wa shamba la vijana wa Kibaha mjini lililopo Boko Timiza. 13 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 16 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutokwa kwa  Dr. Peter Dattan Mkurugenzi wa Shughuliza Afya katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa mahututi ICU katika hospitali hiyo. 17 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa  Dr. Brayson Kiwele  daktari bingwa wa mifupa  katika hospitali teule ya Tumbi Kibaha alipotembelea chumba cha upasuaji. 18 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF mara baada ya kutembelea katika hospitali teule ya Tumbi. 19 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika ukuta wa tanki la mradi wa maji wa mtaa wa  Muheza mjini Kibaha.  20 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mtaa wa Muheza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo, aliyesimama juu ni Grace Lyimo Mhandisi wa maji wa wilaya ya Kibaha. 21 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiakiwa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwinshehe Mlao. 22 
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza kushoto akiwa  na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Pwani  katikati ni Imani Madega Mlezi wa CCM mkoa wa Pwani.

23 
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mh. Silvestry Koka wakionyesha vyeti vyao baada ya kutambuliwa na uongozi wa CCM mkoa wa Pwani kwa mchango wao wanaoutoa kwa CCM Pwani

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »