Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa nasaha fupi katika hafla
fupi ya kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao wamestaafu rasmi
Utumishi wa Umma tangu Julai 1, 2014. Hafla hiyo imefanyika leo Septemba
19, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Wastaafu
wa Jeshi la Magereza(katika picha) wakiwa na familia zao wakimsikiliza
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati
akitoa nasaha fupi kwa Wastaafu hao ambao wamestaafu Utumishi wa Umma
tangu Julai 1, 2014.
Kwaya
ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza inayoundwa na Maafisa na Askari wa
Jeshi la Magereza ikitumbuiza kwenye hafla hiyo ya kuwaaga Wastaafu wa
Jeshi la Magereza. Hafla hiyo imefanyika leo mchana Septemba 19, 2014
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishangilia Wimbo Maalum
uliotumbuizwa na kwaya ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika hafla
fupi ya kuwaaga Maafisa na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza ambao
wamestaafu Utumishi wao kwa mujibu wa Sheria tangu Julai 1, 2014.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi zawadi kwa
Sajin Taji wa Jeshi la Magereza, Kessy Ngwengwe(kushoto) ambaye alikuwa
ni Dreva wa Magari ya Viongozi Makao Makuu ya Jeshi Magereza. Askari
huyo amestaafu Utumishi wake wa Umma tangu Julai 1, 2014.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili toka kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la
Magereza(waliosimama mstari wa nyuma) kwenye hafla fupi ya kuwaaga
Wastaafu hao ambao amestaafu Utumishi wao wa Umma tangu Julai 1, 2014(wa
pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice
Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
EmoticonEmoticon