Kocha mkuu wa Prisons, David Mwamwaja ( wa kwanza kulia)
Na
Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
David
Mwamaja hajafanya usajili mkubwa licha ya kikosi chake kupambana hadi dakika ya
mwisho msimu uliopita ili kusalia katika ligi kuu.
Baada
ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ashanti United, 24 April, Tanzania Prisons
ilifanikiwa kubaki katika ligi kuu Bara. Wengi walitaraji timu hiyo ingefanya
usajili mkubwa wakati wa dirisha la usajili kwa kuamini kuwa timu hiyo
inahitaji mabadiliko makubwa.
Haijawa hivyo na Mwamaja ameweza kuhakikisha
mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Amir Omary anatua katika kikosi chake
kwa lengo la kuongeza makali katika safu ya mashambulizi ambayo ilibebwa zaidi
na mshambulizi, Peter Michael na Richard Peter msimu uliopita.
“
Ligi itakuwa ngumu msimu ujao, lakini tunataka kuirudisha juu Tanzania Prisons
kama ilivyokuwa enzi za kina Osward Morris.Nimeongezwa katika timu hii kwa
lengo la kusaidiana na wachezaji waliopo ili kuifanya Prisons kuwa timu bora
msimu ujao.. Tangu nimefika hapa nimepata vitu vingi vipya ndani na nje ya
uwanja. Upendo, ushirikiano na umoja ni mambo yaliyotawala hapa” anasema
mshambulizi, Amir Omary ambaye amesajiliwa akitokea klabu iliyoshuka daraja ya
JKT Oljoro.
Michael
alifunga mabao 12 msimu uliopita, Richard alifunga mabao manne na Amir alifunga
mabao sita katika kikosi cha Oljoro msimu uliopita na mchexzaji huyo wa
Zanzibar Heroes anaamini kuwa umoja wao utawasumbua walinzi wengi msimu wa
2014/15.
“
Ni safu kali ya mashambulizi, kila timu imejiandaa msimu ujao lakini nachoweza
kusema tumejipanga kuhakikisha Prisons inafanya vizuri msimu ujao. Mwalimu yoko
poa na kila mmoja kikosini anafahamu ni kitu gani ambacho kinatakiwa”
EmoticonEmoticon