OKWI.BANDA WASAJILIWA TIMU MBILI-TFF

September 04, 2014


Na Fadha Kidevu Blog
SHIRIKISHO la soka Tanzania TFF,limetoa majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu 14 ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara huku majina ya wachezaji Emmanuel Okwi na Abdi Banda yakitokea kwenye timu mbili.

Jina la Okwi linatokea kwenye usajili wa timu za Simba na Yanga ilhali jina la beki wa kushoto Banda,limetokea kwenye usajili wa Coastal Union na Simba .

Fadha Kidevu ilijaribu kuwatafuta viongozi wa TFF,wanaoshuhulika na maswala ya usajili ili kutaka kujua sakata hilo na vipi litaamuliwa lakini viongozi hao hawakuweza kupatikana.

Suala hilo linatarajiwa kutolewa uwamuzi baada ya kumalizika kipindi cha mapingamizi ambayo itakuwa ni Septemba 6 kabla ya Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji itakapokutana na kutoa suluhisho la tatizo hilo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »