MKURUGENZI NHC ATEMBELEA ENEO LA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI HALMASHAURI YA BUSOKELO MBEYA

September 04, 2014

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.Nehemia Kyando Mchechu wa kwanza kulia mbele akitembelea eneo la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zitakazojengwa  katika Halmashauri ya Busekelo Mkoani Mbeya alipotembelea Halmashauri hiyo  Septemba 3 mwaka huu .Picha na Saguya wa NHC.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.Nehemia Mchechu akielezea mpango wa shirika wa kujenga nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Busekelo alipotembelea Halmashauri hiyo jana .Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo Bw. Meshack Mwakipunga  na kulia  kwa Mkurugenzi Mkuu wa  NHC ni Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Busekelo Bw Saidi Mderu .
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo Bw,Meshack Mwakipunga akiutembeza ujembe wa shirika la Nyumba la Taifa  kwenye eneo la viwanja vitakavyojengwa  nyumba  na NHC hivi karibuni.
Ujumbe wa NHC na Halmashauri ya Busokelo ukiendelea kutambua  viwanja vitakavyojengwa Nyumba na NHC hivi karibuni
 
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya kuridhia eneo walilopewa na Halmashauri ya Busekelo ili kujenga nyumba hivi karibuni.
Ujumbe ukikagua kazi ya kutengeneza matofali kwa ajili ya kujengea nyumba katika Halmashauri ya Busokelo.
Mhandisi wa  miradi ya nyumba wa NHC Kanda ya Mbeya Bw.Mtili akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa ya ufyatuaji wa matofali ya  kujengea nyumba katika Halmashauri hiyo.
 
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC  ulipata fursa ya kutembelea shamba la mwekezaji wa Kilimo cha Maparachichi baada ya kumaliza ziara yake katika Halmashauri ya Busokelo,ambapo kupitia uwekezaji huo wananchi wa busokelo na maeneo mengine wamepata fursa ya ajira.
Ujembe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukipewa maelezo na Meya wa Jiji la Mbeya Bw.Athanas Kapunga yanayohusu fursa za uwekezaji ambazo NHC inaweza kuzitumia kukuza uchumi wa jiji hilo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »