MICHUANO YA COPA COCA COLA MKOA WA KILIMANJARO KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 23,2014

August 20, 2014
Michuano ya Copa Coca cola ya vijana chini ya miaka 15 kwa mkoa wa Kilimanjaro yanatarajiwa kupigwa Agosti 23 na 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) , Yusuph Mazimu, michuano hiyo itashirikisha kombaini za wilaya zote sita za mkoa huo, 
zilizogawanywa katika makundi mawili, huku wilaya ya Moshi ikiwa na timu mbili .
Kundi la kwanza litakuwa na timu 3 za Wilaya ya Mwanga, Same na Rombo , litakalotumia uwanja wa David Cleopa Msuya uliopo wilayani Mwanga, wakati kundi la pili litakuwa na timu za wilaya ya Moshi Manispaa, Moshi vijijini, Siha na Hai.

Kundi la kwanza litaanza mechi zake Agosti  23, ambapo Mwanga itaanza na Rombo saa 3 asuhubi, baadae saa 6 Mwanga watakipiga na Same, saa 9 alasiri  Same itawavaa Rombo.

Agost 24, vijana wa Moshi Manispaa wataanza kukipiga na Siha saa 3asubuhi, saa 5 Hai na Moshi vijijini, washindi wa mechi hizo watakutana katika mchezo utakaopigwa saa 9 alasiri siku hiyo hiyo.

“Michuano hii inalenga kuunda timu ya mkoa kwa vijana chini ya miaka 15, kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Tanga septemba 9 mwaka huu, tutakapoanzia ugenini, ni muhimu kwa kila wilaya kutumia wachezaji wenye umri unaotakiwa, tutakuwa wakali”, alisema Mazimu.

Mshindi wa jumla kati ya Kilimanjaro na Tanga baada ya kurudiana septemba 13, atafuzu kucheza fainali za copacola taifa zitakazofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Septemba 20 mwaka huu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »