Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila akifungua mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Afisa wa Program wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Kitaifa kutoka Shirika la Afya la Dunia(WHO) Alphonsina Nanai akizungumza jambo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa siku tatu wa magonjwa hayo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Meneja Mpango wa
Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,Dk, Upendo Mwingira (kushoto),
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dk,Neema Rusibamayila(katikati) na kulia ni Afisa wa Program wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Kitaifa kutoka Shirika la Afya la Dunia(WHO) Alphonsina Nanai wakifuatilia mkutano wa tatu wa siku tatu wa magonjwa hayo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Mmoja wadau wa mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome Kanno kutoka (ITI) akijadili jambo leo wakati wa mkutano huo , unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome Kanno, unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome Kanno, unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo - Maelezo
*******************************************
*******************************************
Serikali
inaandaa mpango wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa
kipaumbele(NTD,s) kwa pamoja ili kuweza kufikia watu wengi kwa kupunguza
gharama.
Hayo yamasemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
“ Tumekutana na wadau mbalimbali katika mkutano huu lengo ni tunataka kuandaa mpango wa kutoa huduma na dawa kwa magonjwa yasiyopewa kiupaumbele kwa pamoja badala ya ugonjwa mmoja pekee.Tunaweza kupata matokeo zaidi na kusaidia kuwafikia watu wengi kwa kuwa utarahisisha utendaji kazi, utoaji elimu na dawa,” alisema Dk. Neema.
Dk. Neema aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Aliongeza kuwa hivi sasa huduma hiyo imeweza kufikia wilaya 108 kati ya 160.Hivyo changamoto iliyopo ni kufikia mikoa saba.
Alisema mpango huo ulianza mwaka 2012 na unaendelea hadi mwaka 2017, ambapo mafanikio yameonekana mfano katika
kupambana na ugonjwa wa usubi utafiti ulifanyika umeonesha kuwa kati ya
wilaya tisa ni wilaya mbili ndizo zitaendelea kupatiwa dawa.
Naye Meneja Mpango wa
Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s),Dk, Upendo Mwingira
alisema changamoto nyingine iliyopo katika kubabiliana na magonjwa hayo
ni baadhi ya jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo ambayo
dalili zake si rahisi kuonekana kwa macho kwani huonekana baada ya muda mrefu mfano Matende na Mabusha.
Alisema baadhi ya jamii huwa mwitiko mdogo wakati wa utoaji wa huduma, hivyo Dk. Upendo aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi wakati wa utoaji wa huduma hizo.
Alizitaja baadhi
ya athari ya magonjwa hayo kuwa ni ulemavu wa kudumu na miongoni mwa
sababu zinazochangia kuwepo kwa matataizo hayo ni umasikini.
Dk. Upendo
EmoticonEmoticon