JESHI LA POLISI NIGERIA LATANGAZA DONGE NONO.

May 07, 2014
NA MWANDISHI WETU,ABUJA.

Jeshi la polisi nchini Nigeria limetangaza kitita cha dola za Marekani laki tatu kwa mtu atakaetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa wanafunzi wa kike waliotekwa na Boko Haram.
 
Utekaji wa wanafunzi hao zaidi ya 200 umesababisha vilio ndani na nje ya Nigreia, na kuongeza shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kuwarudhisha wasichana hao. 

Hasira ziliongezeka jana, kufuatia taarifa kuwa wasichana wengine wanane walitekwa kutoka kijiji hicho cha mabli walikotekwa wa awali.

Polisi imeorodhesha nambari sita za simu katika taarifa yao na kuwataka raia wa Nigeria kupiga kwenye nambari hizo kwa taarifa.
Marekani imetuma kundi la  wanajeshi na wataalamu wengine kusaidia upatikanaji w awasichana hao. 

utekaji huo na mashambulizi mengine ya Boko Haram vimeughubika mkutano wa dunia wa kiuchumi kwa bara la Afrika, unaoanza jioni hii mjini Abuja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »