| NAHODHA WA TIMU YA BLACK BURN AMBAO NI MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA NSSF CUP PANGANI AKIPOKEA KOMBE TOKA KWA MKURUGENZI UENDESHAJI NSSF,C,Cresentias Magori . |
NA OSCAR ASSENGA,PANGANI
Timu ya Soka Black Burn FC ya mjini hapa,imetwaa ubingwa wa
kombe la NSSF mwaka 2014 baada ya kuichapa Ushongo FC bao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa kijiji cha Mwera.
| BAADA YA KUKABIDHIWA KOMBE WAKAPIGA PICHA YA PAMOJA. |
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo mbili kuwa na upinzani wa jadi ulishuhudiwa na mamia ya mashabiki walioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa NSSF,Cresentias Magori .
Black Burn ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao Ushongo FC baada ya Farid Nassoro kufunga bao dakika ya 49
lililotokana na shuti lililopita katikati ya walinzi na kumchanganya
mlinda mlango wa Ushongo,Sebastian Charles .
Dakika ya 60 uwanja huo ulilipuka kwa kushangiliwa baada ya
mshambuliaji,Amour Janja kuipatia timu yake ya Usongo FC ambayo ilikuwa ikichezea katika uwanja wake wa nyumbani kupachika wavuni bao la kusawazisha.
| MENEJA WA NSSF MKOA WA TANGA,FRANK MADUGA kulia akipiga picha na mwamuzi bora mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya mpira jana |
Hata hivyo bao hilo halikudumu muda mrefu kwani dakika ya 77 Black Burn iliongeza bao la ushindi kupitia kwa Jumaa Soud ambapo hadi dakika 90 zinamalizika timu hiyo ikatoka kifua mbele kwa bao 2-1.
Kwa ushindi huo,Black burn ilikabidhiwa na Magori kombe,seti ya sare na pesa taslimu sh 200,000 na Usongo ikatwaa seti ya sare n ash 100,000 huku msindi wa tatu Mwera City ikitwaa seti moja ya sare.
Ligi hiyo ya NSSF ilianza Machi 15 mwaka huu kwa kushirikisha timu 14 ambazo zilizoingia nusu fainali ni Ushongo iliyocheza na Urafiki na kuifunga baoa 2-1 huku Blackburn FC nayo ikiifunga Mwera City bao 2-1.
EmoticonEmoticon